Thursday, June 14, 2012

MAMBO YA DOGO JANJA YAKO HAPA!

Jana kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM Msanii Madee wa Tip Top Connection ambae ndio alikabidhiwa na wazazi kumlea na kumsimamia Dogo Janja aliamplfy kuhusu sababu za kumrudisha Dogo Janja mikononi mwa wazazi wake baada ya kudai kumshindwa. Madee kasema “Dogo Janja aliekua form II Makongo High School kakataa kusoma kwa hiyo mimi siwezi kukaa nae wakati hataki kusoma, nilikua safarini Iringa na Mbeya ambapo baada ya kurudi mwalimu wake wa darasa alinipigia simu na kunipa pole kwa sababu Dogo Janja anaumwa, nikashtuka ikabidi nimpigie nikawa simpati kwenye simu.. nikaenda nyumbani kwa Tunda Man alipokuepo na alipojua nimekuja akajificha alikua anataka kunikimbia nikampiga sana vibao, kweli nilimpiga ambapo kesho yake baada ya kuamka nikamuuliza unataka kusoma au kuzurura mtaani? akajibu kwamba anataka kwenda kusoma Arusha ikabidi nimpigie baba yake palepale ambapo mzee wake alniomba nisimrudishe Arusha niendelee kukaa nae” Madee ameendelea kusema kwamba “nilimwacha nyumbani baada ya kuchukua simu yake ambapo nilikuta vitu vingi sana vya kishenzi shenzi kaviandika na ninavyo mpaka leo kwa ajili ya ushahidi, vimeniumiza hasa kwa mtu kama mimi ambae najua nimemtoa wapi, kaandika kuhusu uchafu mbaya na kingine kinanihusu mimi ambacho hapaswi kusema kwa mtu kama yeye, baada ya hapo msimamo wake ulikua vilevile kwamba anataka kurudi kwenda kusoma Arusha, jioni tukakaa kikao juzi na kaka yake na watu wengine na mimi nikampa baraka zote” Kwenye sentensi nyingine Madee amesema “kwa wiki iliyopita na wiki hii Dogo Janja alitoroka kwenda shule kwa siku tatu na hii ni mara ya pili ambapo mara ya kwanza nilimpeleka shule na kumchapa mbele ya wanafunzi wenzake, yani nilivyompeleka shule wanafunzi wenzake mpaka walikua wanamshangaa, alisingizia vitu vingi vya uongo alikua ananidanganya mimi nyumbani na siku hiyo ndio nilimkuta Ubungo Plaza alikua anaogelea na rafiki yake, walimu wake waliniambia hawajamuona shule kwa muda wa wiki moja”

Wednesday, June 13, 2012

DOGO JANJA ARUDISHWA KWAO ARUSHA

Msanii mchanga anayetikisa kwenye anga la muziki wa Bongolfeva kwa staili yake ya HipHop kutoka mkoani Arusha anayejulikana kwa jina maarufu la Dogo Janja arudishwa kwao Arusha. Dogo janja ambaye alikuwa akisoma shule ya sekondari Makongo na alikuwa akisimamiwa kazi zake za muziki pamoja na shule na kundi zima la TipTop chini ya Madee ametuhumiwa kwa tabia mbaya ya utoro shuleni pamoja na kukiuka misingi ya mikataba na kundi hilo hivyo wameamua kumrudisha kwao Arusha kuepuka lawama kutoka kwa wazazi pamoja na jamii kwa ujumla kwani wao ndio waliomleta Dar na waliahidi kusimamia kila kinachomhusu Dogo Janja ikiwemo shule.

Monday, June 4, 2012

JINI LA SARENDA EPISODE 1.

Majira ya saa nane za usiku msichana Suzana alikuwa akitoka kujirusha katika ukumbi wa Bilicanas. Kilichomshtua kilikuwa kutoweka kwa mpenzi wake Sammy ambaye aliondoka bila kumuaga. Wazo lake la kwanza lilikuwa Sammy kaondoka na msichana mwingine akijua kabisa yeye ndiye mchumba wake. Akiwa amekasirika kwa kitendo cha Sammy kuondoka na kumuacha peke yake, kila alipopiga simu yake iliita bila kupokelewa kitu kilichoonesha dharau. Aliamua kurudi nyumbani kwake japo alipanga siku ile kwenda kulala kwa Sammy. Aliendesha gari akiwa amefura kwa hasira huku machozi yakimtoka kutokana kitendo alichotendewa na mpenzi wake ambaye ndiye aliyemtoa kitandani alipokuwa amekwisha kulala. Suzana awaliza mengi juu ya kitendo cha mpenzi wake kumwita klabu na kumkimbia. Wakati akitoka Bilicanas mvua ilianza kunyesha, hakutaka kuisubiri aliamua kwenda nayo ili awahi kunyumba angalau alale kwa muda mchache ili asubuhi awahi kanisani misa ya kwanza. Mvua ilikuwa kubwa iliyoambatana na upepo mkali kitu kilichomfanya ashindwe kuona mbele ilimbidi alisimamishe gari pembeni ya daraja ya Salenda ili kusubiri upepo upungue ndipo aendelee na safari yake. Upepo ule haukuchukua ulitulia na mvua ilikuwa imekatika. Alipowasha gari liligoma kuwaka, alirudia zaidi ya mara tano kuzungusha funguo lakini liligoma kuwaka. Kuteremka kwenye gari alishindwa kutokana na hali ya kiza cha kutisha nje. Wasi wasi ulimtawala na kujiuliza atatokaje pale au ndio atalala mpaka asubuhi. Hasira zilizidi kumpanda Suzana kutokana na kukimbiwa na mpenzi wake na kuharibikiwa na gari. Kutokana na hofu aliyokuwa nayo alihakikisha milango na vioo vyote vimefungwa vizuri. Alijikuta akipiga dua kumuomba Mungu amuokoe la janga lile kwa kupata msaada wa watu wenye gari kumsaidia kuwasha gari lake. Lakini kwa muda ule hakukuwa na dalili ya gari lolote kupita. Akiwa ameinama mikono ameikutanisha kifuani kwake alishtushwa na upepo makali uliovuka toka baharini na kulifanya gari lake kuyumba na kusogea kidogo. Kwa woga uliompata Suzana alijikuta akitokwa na haja ndogo bila kuelewa. Alitamani kulia lakini aliamini sauti yake haitasaidia lolote kwa vile hakukuwa na wakumsaidia. Aliinama kwa woga hakutaka kuangalia popote zaidi ya kusubiri chochote kitakachomtokea. Baada ya muda hali ile ilitulia, Suzana alinyanyua kichwa taratibu ili achukue simu ampigie baba yake amfuate eneo lile ambalo lilikuwa limemuweka katika hali ya hatari. Aliponyanyua uso achukue simu iliyokuwa kwenye kwenye dash board, alishtushwa na mwanga mkali kama jua la saa saba mchana. Aliangalia katikati ya bahari palipokuwa kunatoka mwanga ule. Alituliza macho baada ya kumuona mwanamke aliyekuwa amevaa gauni jeupe lilikuwa liking’aa kutokana na mapambo yake. Hali ile ilimfanya asahau yalitomtokea muda mfupi na kutuliza macho kumuangalia yule mwanamke aliyekuwa akitembea juu ya maji huku nyuma akisindikizwa na wasichana walikuwa wamebeba vikapu vidogo vilivyokuwa na maua ambayo walimwagia kila hatua ilivyopigwa huku wakiimba nyimbo nzuri. Suzana alijikuta akipata ujasiri wa ajabu kwa kufungua dirisha kidogo ili aweze kusikia watu wale walikuwa wakiimba kitu gani. Zilikuwa sauti nzuri kama za kaswida zilizoibwa kwa lugha ya kiarabu. Nyimbo zile zilimvutia na kujikuta akiwa na hamu ya kuwaona watu wale waliokuwa wakitembea juu ya maji huku kwa mstari mbele akitangulia yule mwanamke ambaye usoni kwake kulikuwa kunawaka kama taa na kushindwa kuiona sura yake vizuri. Suzana alijikuta akisahau kama wale watu walikuwa wakitembea juu ya maji zaidi ya kushangazwa na sherehe ile ambayo toka azaliwe hajawahi kuona sherehe ya aina ile ya mtu mmoja kutangulia mbele wengine kumfuata nyuma huku wakimuwagia maua na kumwimbia nyimbo nzuri. Baada ya muda watu wote walikaa mstari mmoja, kisha yule mwanamke aliyekuwa amepeneza kuliko wote alipita katikati yao na kupigiwa vilegele huku akitupiwa maua. Manukato ya maua yalisambaa mpaka ndani ya gari la Suzana alilokuwa amefungua kioo kidogo kusikia nyimbo alizokuwa anaimbiwa yule mwanamke ambaye alionekana kama bibi harusi lakini muda wote hakumuona bwana harusi wala mwanaume kwenye kundi lile. Yule mwanamke alipita kwenye mstari mpaka mwisho alitembea peke yake bila kufuatwa na mtu kisha aligeuka na kuwapungia mkono wenzake ambao nao walimpungia huku wakimrushia maua. Baada ya kutembea kidogo Suzana alimshuhudia yule mwanamke alikunja gauni lake usawa na kifua na kushangaa kumuona akitembea ndani ya maji yaliyokuwa yamemfika tumboni. Suzana alijikuta akishtuka na kujiuliza yupo ndotoni au anaona kweli, kilichomshangaza ni umbali aliotoka yule mwanamke akitembea juu ya maji. Lakini cha kushangaza alipokaribia ufukweni alionekana yupo ndani ya maji yaliyomfikia tumboni. Aliendelea kumtazama amuone anakwenda wapi, yule mwanamke baada ya kutoka ndani ya maji alitembea juu ya mchanga kulifuata lile gari. Kila hatua ilivyokuwa akipiga ilizidi kumtisha Suzana, alijikuta akimshangaa kutaka kuijua sura yake. Alituliza macho yake kwenye uso wa yule mwanamke aliyekuwa akiisogelea gari huku manukato makali yakizidi kujaa ndani ya gari. Kilichomshangaza zaidi ni sura ya yule mwanamke alikuwa akifanana naye kwa kila kitu umbile na sura. Suzana alishtuka na kufunga kioo haraka ili mtu yule ambaye yeye alimuona wa muujiza asiingie kwenye gari. Yule mwanamke alisogea kwenye gari na kuligusa, ajabu baada ya kuligusa lile gari alitoweka ghafla. Suzana akiwa anatetemeka alijaribu kuwasha gari kwa mara nyingine, ajabu ya Mungu gari liliwaka aliondoka eneo lile kwa mwendo wa kasi. Alipofika nyumbani kulikuwa kumekucha, alikwenda kuoga haraka ili awahi kanisani kwani muda ulikuwa umekwenda. Baada ya kuoga alirudi ndani, lakini alishtushwa na harufu ya manukato ambayo aliyasikia muda mfupi darajani gari lake lilipozima na kuenea hadi ndani ya gari lake. Hakutaka kulifikiria sana lile kwa muda ulikuwa umekwenda, alikwenda kwenye kabati kubadili nguo ili awahi kanisani. Baada ya kumaliza kubadili nguo alijikuta akiingiwa na uvivu na kwenda kukaa kwenye kitanda haikupita muda. Usingizi mzito ulimshika na kulala bila kujielewa, aliposhtuka usingizini alishtuka kuiona familia yake yote imesimama mbele yake. Alijiuliza kuna nini, alipojiangalia alijiona alikuwa amevaa nguo za kuendea kanisani. “Suzana upo sawa?” Mama yake alimuuliza. “Mbona unaniuliza hivyo? Halafu mbona kama wote mlikuwa mnalia kuna nini mbona mnanitisha? Nini kimemtokea Suzana mpaka familia yake ikusanyike mbele yake huku wakitokwa na machozi. Kuyajua yote fuatana nami katika simulizi hii mpya ya kusisimua

Tuesday, May 29, 2012

FARU WA KWENYE PROJECT YA SERENGETI

Kusema Ukweli Nimepokea Kwa Masikitiko Habari Ya Kuwa Maasikari Walioshiriki Kuua Faru 2 Wa Kwenye Project ya Serengeti Ukizingatia Faru Ni Kati ya Wanyama Walio Hatarini Kupotea Kabisa Kizazi Hivi Mnatutakia Nini Wale Ambao Tumesomea Wanyama Pori Mnataka Tujipatie Wapi Riziki Au Mtatupatia Hakuna Kitu kina Niudhi Kama Mtu Anayeshiriki Kusababisha Kifo Cha Mti,Nyasi,Wadudud Wanyama Kwa Maslahi Yao Binafsi Naomba Hao Watu Walioshiriki Katika Vifo Vya Hao Faru 2 Wawajibishwe Kwani Wanyama Hawa Ni Moja Kati Ya Vivutio Vikubwa Tanzania na Dunia Isitoshe Ni Adimu Yaani Isitoshe Nchi Nyingine Hawana Faru KAMA HIYO HAITOSHE HAWA WANYAMA HARUHUSIWI KUWINDWA