Thursday, June 14, 2012
MAMBO YA DOGO JANJA YAKO HAPA!
Jana kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM Msanii
Madee wa Tip Top Connection ambae ndio
alikabidhiwa na wazazi kumlea na
kumsimamia Dogo Janja aliamplfy kuhusu
sababu za kumrudisha Dogo Janja mikononi
mwa wazazi wake baada ya kudai kumshindwa. Madee kasema “Dogo Janja aliekua form II
Makongo High School kakataa kusoma kwa
hiyo mimi siwezi kukaa nae wakati hataki
kusoma, nilikua safarini Iringa na Mbeya
ambapo baada ya kurudi mwalimu wake wa
darasa alinipigia simu na kunipa pole kwa sababu Dogo Janja anaumwa, nikashtuka
ikabidi nimpigie nikawa simpati kwenye simu..
nikaenda nyumbani kwa Tunda Man
alipokuepo na alipojua nimekuja akajificha
alikua anataka kunikimbia nikampiga sana
vibao, kweli nilimpiga ambapo kesho yake baada ya kuamka nikamuuliza unataka
kusoma au kuzurura mtaani? akajibu kwamba
anataka kwenda kusoma Arusha ikabidi
nimpigie baba yake palepale ambapo mzee
wake alniomba nisimrudishe Arusha niendelee
kukaa nae” Madee ameendelea kusema kwamba
“nilimwacha nyumbani baada ya kuchukua
simu yake ambapo nilikuta vitu vingi sana vya
kishenzi shenzi kaviandika na ninavyo mpaka
leo kwa ajili ya ushahidi, vimeniumiza hasa
kwa mtu kama mimi ambae najua nimemtoa wapi, kaandika kuhusu uchafu mbaya na
kingine kinanihusu mimi ambacho hapaswi
kusema kwa mtu kama yeye, baada ya hapo
msimamo wake ulikua vilevile kwamba
anataka kurudi kwenda kusoma Arusha, jioni
tukakaa kikao juzi na kaka yake na watu wengine na mimi nikampa baraka zote” Kwenye sentensi nyingine Madee amesema
“kwa wiki iliyopita na wiki hii Dogo Janja
alitoroka kwenda shule kwa siku tatu na hii ni
mara ya pili ambapo mara ya kwanza
nilimpeleka shule na kumchapa mbele ya
wanafunzi wenzake, yani nilivyompeleka shule wanafunzi wenzake mpaka walikua
wanamshangaa, alisingizia vitu vingi vya
uongo alikua ananidanganya mimi nyumbani
na siku hiyo ndio nilimkuta Ubungo Plaza
alikua anaogelea na rafiki yake, walimu wake
waliniambia hawajamuona shule kwa muda wa wiki moja”
No comments:
Post a Comment